Msaada

Kituo cha Msaada

Majibu ya maswali ya kawaida kuhusu Kitabuni. Huoni jibu unalotafuta? Wasiliana nasi moja kwa moja hapa chini.

Akaunti na Usajili

Ninawezaje kujiunga na Kitabuni?

Bofya "Jiunge" juu ya ukurasa, jaza jina la mtumiaji na nywila, kisha ujaze jina la biashara yako kwenye akaunti yako baadaye. Huduma nyingi (kama Lugha na Jifunze) zina kipindi cha majaribio ya bure kabla ya kuhitaji kulipia. (akaunti yako)

Nimesahau nywila yangu, nifanye nini?

Nenda kwenye ukurasa wa Umesahau Nywila. Kama namba yako ina WhatsApp, utatumiwa msimbo (OTP) wa kuthibitisha huko; au chagua kupokea msimbo kwenye barua pepe uliyosajili (unaweza kuiweka kwenye ukurasa wa Akaunti Yangu). Kama huna WhatsApp wala barua pepe, utaelekezwa hapa kwenye Msaada ili msimamizi akuthibitishe na kukusaidia kubadilisha nywila - unaweza pia kumuuliza Ramadhan (chini ya ukurasa huu) akuelekeze.

Nawezaje kufuta akaunti yangu?

Kwenye ukurasa wa Akaunti Yangu kuna kitufe cha "Futa Akaunti" chini kabisa. Kitendo hiki hakiwezi kutenguliwa. (Akaunti Yangu)

Malipo na Vifurushi

Ninalipaje huduma?

Nenda /vifurushi, chagua huduma unayotaka na muda (siku au mwezi), kisha "Nunua" kutakupeleka kwenye ukurasa salama wa malipo. Ufikiaji unafunguliwa moja kwa moja baada ya malipo kukamilika.

Nimelipa lakini ufikiaji haujafunguka, nifanye nini?

Mara nyingi hii huchukua sekunde chache tu. Ukisubiri zaidi ya dakika chache bila mabadiliko, wasiliana nasi (chini ya ukurasa huu) ukiwa na risiti/order number yako ili tukusaidie haraka.

Nikimwalika rafiki, napata nini?

Wewe na rafiki yako mnapata siku 7 za bure za huduma anayolipia mara ya kwanza. Pata kiungo chako cha kualika kwenye Alika Rafiki.

Huduma Zetu

Kitabuni ina huduma gani?

Tunatoa: Lugha (mazungumzo ya AI), Programu/Jifunze (kozi za IT, Biashara na Ajira), QR Menu (menyu ya mkahawa/hoteli), Duka la Mtandaoni, na Booking (uhifadhi wa meza/chumba). Kila moja ina ukurasa wake wa dashibodi baada ya kuingia.

Biashara yangu inawezaje kuonekana kwenye Saraka?

Nenda kwenye Akaunti Yangu, weka jina la biashara na eneo lako, kisha washa "Onyesha biashara yangu kwenye Saraka". Biashara lazima iwe na huduma moja hai (QR Menu, Duka au Booking) ili ionekane.

Nawezaje kuongeza mfanyakazi wa kusimamia oda?

Kwenye dashibodi ya huduma yako (QR Menu, Duka au Booking) tafuta kiungo cha "👥 Wafanyakazi". Mfanyakazi anaweza kuona na kusasisha hali ya oda pekee - hana ufikiaji wa malipo au mipangilio.

💬 Ongea na Ramadhan

Muulize chochote - hata kama huwezi kuingia kwenye akaunti yako.

Habari! Mimi ni Ramadhan. Naweza kukusaidiaje leo?

Ujumbe uliobaki leo: 20 / 20